21 Juni 2025 - 13:34
Sheikh al-Azhar, Ahmad al-Tayeb, amelaani vikali mashambulizi ya uchokozi ya Israel dhidi ya Iran

Kimya cha jumuiya ya kimataifa kuhusu uonevu na uchokozi huu na kukosekana kauli za kuuzuwia, kinachukuliwa kuwa ni ushiriki katika jinai hizo, na matokeo yake pekee yatakuwa ni tishio kwa usalama wa dunia nzima. Vita havizai amani."

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Katika ujumbe aliouchapisha kwenye ukurasa wake wa Facebook uliotolewa kwa lugha za Kiarabu na Kifarsi, amesema:  

"Ninalaani kwa nguvu uvunjaji wa mara kwa mara wa utawala vamizi wa Kizayuni dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na mashambulizi ya uchokozi na ukatili usiokoma wa utawala huu ghasibu na mhalifu, ambao unalenga kupeleka eneo hili zima la kikanda karibu na kona ya kulipuka kwa vita vya jumla vinavyoleta faida kwa wafanyabiashara wa damu na silaha pekee".

Kimya cha jumuiya ya kimataifa kuhusu uonevu na uchokozi huu na kukosekana kauli za kuuzuwia, kinachukuliwa kuwa ni ushiriki katika jinai hizo, na matokeo yake pekee yatakuwa ni tishio kwa usalama wa dunia nzima. Vita havizai amani."

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha